Uchaguzi wa Tanzania 2020: Mahakama ya Afrika yataka Tanzania kuruhusu kupingwa kwa matokeo ya urais mahakamani Saa 1 iliyopita CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Mahakama ya tanzania hairuhusu matokeo ya uchaguzi kupingwa mahakamani Mahakama ya Afrika imeamuru Tanzania kuviruhusu vyama vya siasa kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais mahakamani Katiba ya Tanzania hairuhusu mahakama kuhoji wala kupinga matokeo ya urais mara mshindi wa uchaguzi atakapokuwa ametangazwa na tume ya uchaguzi Lakini jana, Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, yenye makao yake makuu jijini Arusha, Kaskazini mwa Tanzania, imeitaka Tanzania kuchukua hatua "za muhimu za kikatiba na za kisheria, ndani ya muda mwafaka" kubadilisha sheria hiyo inayozuia kupingwa kwa matokeo ya urais Kesi hii ilipelekwa mahakamani hapo na Mtanzania na mwanasheria nguli wa haki za binadamu Jebra Kambole ambaye alihoji kwamba kifungu hicho cha sheria kinachozuia kupingwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais ...
Posts
Showing posts from July, 2020