Posts

Image
Uchaguzi wa Tanzania 2020: Mahakama ya Afrika yataka Tanzania kuruhusu kupingwa kwa matokeo ya urais mahakamani Saa 1 iliyopita CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Mahakama ya tanzania hairuhusu matokeo ya uchaguzi kupingwa mahakamani Mahakama ya Afrika imeamuru Tanzania kuviruhusu vyama vya siasa kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais mahakamani Katiba ya Tanzania hairuhusu mahakama kuhoji wala kupinga matokeo ya urais mara mshindi wa uchaguzi atakapokuwa ametangazwa na tume ya uchaguzi Lakini jana, Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, yenye makao yake makuu jijini Arusha, Kaskazini mwa Tanzania, imeitaka Tanzania kuchukua hatua "za muhimu za kikatiba na za kisheria, ndani ya muda mwafaka" kubadilisha sheria hiyo inayozuia kupingwa kwa matokeo ya urais Kesi hii ilipelekwa mahakamani hapo na Mtanzania na mwanasheria nguli wa haki za binadamu Jebra Kambole ambaye alihoji kwamba kifungu hicho cha sheria kinachozuia kupingwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais ...

Diamond platinumz na maajabu yake YouTube

Image
Diamond Platnumz analinganishwaje na nyota wengine wa Afrika katika mtandao wa YouTube? 16 Juni 2020 Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii WhatsApp   Sambaza habari hii Messenger   Sambaza habari hii Twitter   Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha WCB_WASAFI Diamond Platinumz alishangazwa na wazalishaji wake wa muziki wiki iliopita walipoingia katika nyumba yake na keki iliokuwa na nembo ya kuadhimisha hatua muhimu ya nyota huyo wa Tanzania. Huku akipigwa picha akivalia nguo , mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 30 aliambiwa na kundi lake kwamba ndiye msanii wa kwanza katika jangwa la sahara kupata views bilioni moja katika chaneli ya Youtube

UBAGUZI

Image
Burnely yatiwa aibu kwa bango la ubaguzi wa rangi uwanjani 23 Juni 2020 Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii WhatsApp   Sambaza habari hii Messenger   Sambaza habari hii Twitter   Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Burnley wameaibika baada ya bango lililokuwa na maneno 'Maisha ya wazungu ni muhimu Burnley' kupeperushwa na ndege moja katika uwanja wa Etihad wakati wa mechi ya Jumatatu kati ya Burnely na Manchester City. Ndege hiyo ilizunguka mara kadhaa juu ya uwanja baada ya mchuano huo kuanza ambapo City aliichabanga Burnley mabao 5 kwa nunge. Awali, wachezaji wa Burnley na City na wafanyakazi walikuwa wamepiga goti kuunga mkono harakati za vuguvugu la Black Lives Matter. "Mashabiki wa aina hiyo hawastahili kuwa uwanjani," Ben Mee ameiambia BBC Radio 5 Live. Mlinzi Mee ameongeza: "Tumeaibishwa, Tumefadhaishwa. "Ni wale mashabiki wetu kidogo - Najua ninazungumza kwa niaba ya mashabiki wetu wengi wanaojitenga na mambo kama haya...

News

Image
Kim Jong-un 'aahirisha hatua za kijeshi' Korea Kusini   24 Juni 2020 Sambaza habari hii Email   Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii Twitter   Sambaza habari hii Whatsapp Image copyright GETTY IMAGES Image caption Kim Jong-un and South Korea's Moon Jae-in in better days Korea Kaskazini imeahirisha "hatua za kijeshi"dhidi ya Korea Kusini, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya taifa hilo. Wiki za hivi karibuni ilishuhudiwa kuongezeka kwa maneno ya hasira kutoka kwa Korea Kaskazini juu ya mipango ya mwanaharakati ya kutuma vijikaratasi vilivyokua vimechapishwa jumbe za kuipinga Korea Kaskazini kuhusiana na mpaka. Wiki iliyopita Korea Kaskazini ililipua ofisi inayotumiwa na kwa pamoja na Korea mbili na pia ikatishia kutuma vikosi vyake kwenye eneo la mpaka wa nchi hizo. Lakini katika mkutano ulioongozwa na Kim Jong-un, uamuzi ulichukuliwa wa kuahirisha hatua ya kijeshi, kulingana na vyombo vya habari vya taifa. Kwanini Korea Kaskazini ililipua ofisi ya mawas...

MATUMIZI YA DAWA

Image
Matumizi ya dawa za dharura kuzuia mimba na mipira ya kiume yapungua Uingereza   24 Juni 2020 Sambaza habari hii Email   Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii Twitter   Sambaza habari hii Whatsapp Image copyright GETTY IMAGES Amri ya kutotoka nje imesababisha kupungua kwa mauzo ya vidonge vya kuzuia mimba ambazo hutumika mara tu baada ya kujamiiana maarufu kama (morning-after pills), utafiti umeonesha. Takwimu zinaonesha mauzo yalipungua kwa asilimia 50 kuanzia Machi hadi Aprili, huku idadi ya wanaokwenda kuandikiwa dawa hiyo hospitali nchini Uingereza ikipungua kwa karibu asilimia 20. Huduma ya ushauri wa masuala ya uzazi Uingereza, imesema takwimu hiyo inaonesha haja ya dawa hizo kuanza kuuzwa katika maduka ya jumla bila kuhitaji karatasi ya daktari. Serikali imesema mabadiliko yoyote ya sheria lazima yafikie kiwango cha usalama kinachohitaji. Tofauti na nchi zenye mfumo mwingine wa afya kama Afrika Mashariki ambapo dawa hizi za kuzuia mimba punde tu baa...