Skip to main content

News

Kim Jong-un 'aahirisha hatua za kijeshi' Korea Kusini

  •  
   

Image copyrightGETTY IMAGESKim Jong-un, Moon Jae-in and Kim Yo-jong
Image captionKim Jong-un and South Korea's Moon Jae-in in better days

Korea Kaskazini imeahirisha "hatua za kijeshi"dhidi ya Korea Kusini, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya taifa hilo.

Wiki za hivi karibuni ilishuhudiwa kuongezeka kwa maneno ya hasira kutoka kwa Korea Kaskazini juu ya mipango ya mwanaharakati ya kutuma vijikaratasi vilivyokua vimechapishwa jumbe za kuipinga Korea Kaskazini kuhusiana na mpaka.

Wiki iliyopita Korea Kaskazini ililipua ofisi inayotumiwa na kwa pamoja na Korea mbili na pia ikatishia kutuma vikosi vyake kwenye eneo la mpaka wa nchi hizo.

Lakini katika mkutano ulioongozwa na Kim Jong-un, uamuzi ulichukuliwa wa kuahirisha hatua ya kijeshi, kulingana na vyombo vya habari vya taifa.

Tume ya kijeshi ilichukua uamuzi wake baada ya kile ilichokiita kuzingatia "hali iliyojitokeza"

Korea Kaskazini pia ilianza kuharibu vipazasauti ilivyokua imeviweka wiki jana tu, ambavyo kwa kawaida hutumiwa kupinga jumbe za kupinga Korea Kaskazini kwenye mpaka, Yonhap iliripoti.

Ilionyesha ghadhabu yake kwa maneno makali baada ya dada yake Kim , Kim Yo-jong kuamuru jeshi "kuchukua hatua kali zinazofuata ". - kwa upande mmoja kwasababu ya kile ambacho Pyongyang ilisema ni kushindwa kwa Seoul kuwazuwia wanaharakati kutundika baluni zenye vijikaratasi vya kupinga utawala wa Korea Kskazini kwenye mpaka.

Mkutano pia ulijadili kuhusu nyaraka zinazoainisha hatua za "kuimarisha juhudi za kuzuwia vita vya nchi ,"Shirika la habari la taifa KCNA liliripoti.

Presentational grey line

UCHAMBUZI

Ilionekana kama karatasi iliyokuwa imeandikwa. Sera ya hatari ya Korea Kaskazini kwa ajili ya kulinda maslahi ya usalama bila kikomo ilikua imerejeshwa.

Kulipua ofisi ya mawasiliano inayotumiwa nan chi mbili ilikua ni hatua ya kwanza tu tuliyoambiwa na utawala wa Pyongyang. Dada yake kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Yo-Jong alikua ameagiza jeshi kuandaa mpango.

Lakini kwa wale walioangalia kwa uangalifu, kulikua wakati wote na kipengele cha nje.

Wakati jeshi la Korea Kaskazini lilipotangaza kuwa linaandaa mpango, taarifa ilitaja kwamba mipango hiyo itatakiwa kuidhinishwa na makao makuu ya jeshi.

Kwa maana nyingine, Kim Jong-Un atatakiwa kuwa na usemi wa mwisho.

Je ni kwanini aliamua kuondoa mpango huo?

Baadhi ya wachambuzi wameelezea kuwa kuna uwezekano kwamba Bwana Kim anaweza kujifanya askari mbaya wa dada yake kabla ya mazungumzo yajyayo. Kumbuka, mipango ya kijeshi ya hatua za kijeshi- sio kufuta kwa hiyo bado kuna uwezekano.

Hali hii ya uhasama bila shaka imempa Kim-Yo-Jong fursa thabiti ya kuonyesha aina ya uongozi wake, lakini bado tunafahamu ni nani ambaye bado ana mamlaka.

Kim Jong-un kwa sasa anaweza kuwa na kama kiongozi mzuri ambaye yuko tayari kusamehe na kutuliza hali ya uhasama. Inaweza kumfanya aonekane mtu mwema ndani ya nchi.

Ninachoweza kusema ni kwamba hakukosi mambo katika rasi ya Korea na kwa sasa walau, utawala wa Rais Moon mjini Seoul utakua na ahueni kwa muda .

Comments

Popular posts from this blog

MATUMIZI YA DAWA