Matumizi ya dawa za dharura kuzuia mimba na mipira ya kiume yapungua Uingereza 24 Juni 2020 Sambaza habari hii Email Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Whatsapp Image copyright GETTY IMAGES Amri ya kutotoka nje imesababisha kupungua kwa mauzo ya vidonge vya kuzuia mimba ambazo hutumika mara tu baada ya kujamiiana maarufu kama (morning-after pills), utafiti umeonesha. Takwimu zinaonesha mauzo yalipungua kwa asilimia 50 kuanzia Machi hadi Aprili, huku idadi ya wanaokwenda kuandikiwa dawa hiyo hospitali nchini Uingereza ikipungua kwa karibu asilimia 20. Huduma ya ushauri wa masuala ya uzazi Uingereza, imesema takwimu hiyo inaonesha haja ya dawa hizo kuanza kuuzwa katika maduka ya jumla bila kuhitaji karatasi ya daktari. Serikali imesema mabadiliko yoyote ya sheria lazima yafikie kiwango cha usalama kinachohitaji. Tofauti na nchi zenye mfumo mwingine wa afya kama Afrika Mashariki ambapo dawa hizi za kuzuia mimba punde tu baa...
Comments
Post a Comment